Taarifa hiyo ya HAMAS imesema: "Baada ya kufanya uhalifu mpya kwa kuishambulia kwa mabomu Hospitali ya Al Mamadani na kupelelekea kusimamishwa huduma zote za hospitani hiyo, jeshi vamizi la Israel linadai kuwa eti eneo hilo lilikuwa linatumika katika mambo ya kijeshi." Uongo huu wa wazi ni marudio ya madai ambayo yamekuwa yakitolewa na adui Mzayuni tangu awali ili kujaribu kuhalalisha jinai zake za kushambulia makazi ya watu pamoja na kushambulia raia na vituo vya matibabu kama Kituo cha Matibabu cha Shifa.
Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imeonesha kukasirishwa sana na jinai za kutisha zilizofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Hospitali ya Al-Mamadani huko Ghaza.
Shirika la Habari la Mehr limenukuu taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ikilaani jinai za kutisha za utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo vya matibabu hususan uhalifu wake wa kushambulia kwa makusudi Hospitali ya Al-Mamadani huko Ghaza na kuonya kuhusu hatari za kusambaratika kikamilifu mfumo wa huduma za afya wa Ghaza na kuenea ghasia katika eneo hilo kutokana na vitendo vya kutisha vinavyoendelea kufanywa na Israel.
Katika taarifa hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imeitaka jamii ya kimataifa kutekeleza wajibu wake wa kuwalinda raia wa Ghaza.
342/
Your Comment